Jumanne, 22 Agosti 2017 14:45

UWEKAJI WA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MAABARA -TAEC.

Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara ya kisasa ya Teknolojia ya nyuklia, kwenye Tume ya nguvu za Atomiki, wengine walioshiriki uzinduzi huo ni Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Katibu Mkuu Profesa Saimon Msanjila na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako akiweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara ya kisasa ya Teknolojia ya nyuklia, kwenye Tume ya nguvu za Atomiki, wengine walioshiriki uzinduzi huo ni Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Katibu Mkuu Profesa Saimon Msanjila na Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako leo ameweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara ya  Teknolojia ya Nyuklia kwenye Tume ya Nguvu za Atomiki nchini (TAEC), mkoani Arusha, maaabara ambayo inatarajiwa kuwa kubwa na ya kisasa kwa vifaa barani Afrika.

Akizungumza na viongozi mbali mbali wa mkoa huo na watumishi wa taasisi hiyo Waziri Ndalichako amesema maabara hiyo ni ya watanzania na hivyo watumishi wanaofanya kazi katika tume hiyo  wasifanye kazi kwa ubinafsi na badala yake watangulize maslahi ya Taifa mbele.

Majengo ya Maabara hiyo ya kisasa yanatarajiwa kukamilika Februari Mwaka 2018 ambapo yatagharimu kiasi cha shilingi   Bilioni 2.3, na ikikamilika Umoja wa Ulaya itafunga vifaa vyenye thamani ya Sh. Bilioni 11 ambapo  tayari baadhi ya vifaa vya Sh. Bilioni 2.6 vimekwishawasili nchini.

Pia waziri na viongozi wengine wa wizara wametembela Chuo cha Veta sehemu ya kuzalishia umeme kikuletwa pamoja na Chuo cha Ualimu Elimu Maalumu Patandi, kwa lengo la kukagua miundombinu ya Chuo hicho pamoja kujionea vifaa vya kufundishia wanafunzi wenye mahitaji maalumu.

Viongozi wengine ambao waliambatana na waziri kwenye ziara hiyo ni pamoja na Naibu waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia  Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Katibu Mkuu Profesa Saimon Msanjila.

Read 1577 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…