Jumatatu, 14 Agosti 2017 18:08

WAZIRI NDALICHAKO:WANAFUNZI SOMENI KWA BIDII NA WALIMU FANYENI KAZI KWA WELEDI.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndakichako amewataka wanafunzi wa shule ya Sekondari Mwinyi na ile ya Nasibugani kuhakikisha
wanasoma kwa bidii, na kuacha kujiingiza kwenye vikundi au mambo ambayo hayana tija kwa maendeleo ya Taifa.
 
 Waziri Ndalichako ameyasema hayo leo wakati alipofanya ziara wilayani Mkuranga mkoani Pwani kwa lengo la kukagua ujenzi unaoendelea wa vyumba vya madarasa, mabweni na matundu ya vyoo katika shule hizo chini ya programu ya Lipa kulingana na matokeo.
 
Profesa Ndalichako amesema Jitihada zinazofanywa na Rais John Magufuli za kuhakikisha Elimu bora inatolewa kwa wanafunzi zinapaswa kuungwa mkono kwa kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake ipasavyo ikiwa ni pamoja na wanafunzi kufaulu vizuri.
 
Waziri Ndalichako amesisitiza kuwa Serikali Haihitaji kuona wanafunzi wanafeli bali  inataka kuona wanafunzi wanafaulu ambapo  amewasihi walimu kutimiza majukumu yao kwa kuzingatia weledi. 
 
Katika ziara hiyo waziri Ndalichako amezindua mabweni katika shule ya Sekondari Mwinyi na kuweka jiwe la msingi ujenzi wa mabweni katika shule ya Sekondari Nasibugani.

 

Read 9239 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: Block 10
  •               College of Business Studies and Law
  •               University of Dodoma (UDOM)
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…