Alhamisi, 10 Agosti 2017 13:38

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia yapokea msaada wa vitabu vya sayansi kutoka India.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo imepokea vitabu vya masomo ya Sayansi na Hisabati milioni moja na thelathini elfu toka serikali ya India kupitia balozi wake Saandep Arya

vitabu ambavyo vitatumika kwa wanafunzi wa kidato cha Tatu mpaka cha Sita.

Akizungumza wakati wa kupokea vitabu hivyo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako amesema serikali ya awamu ya Tano kipaumbele chake ni kuhakikisha Elimu bora inapatikana, kwamba sayansi ndiyo kipaumbele  ili Taifa liweze kufikia malengo yake ya kuwa na uchumi wa viwanda.

Profesa Ndalichako amesema kuwa Taifa la India limepiga hatua katika masula ya Teknolojia hivyo kupitia mahusuiano  mema yaliyopo kati ya nchi hizo yataifanya Tanzania kufikia malengo yake, ambapo tayari walimu hamsini wa masomo ya sayansi toka nchini India tayari wameanza kazi ya kufundisha wanafunzi katika shule mbalimbali nchini.

Vitabu hivyo vinahusisha masomo ya fizikia, kemia, baiolojia na hisabati na kipaumbele kitakuwa ni kwenye shule ambazo zinamazingira magumumu katika kuzifikia.

Read 6448 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…