Jumatano, 09 Agosti 2017 18:36

WANAFUNZI WA MASOMO YA SAYANSI WATAKIWA KUSOMA KWA BIDII

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Simon Msanjila amewataka wanafunzi kusoma  kwa bidii, na walimu kufanya kazi kwa kuzingatia maadili

na miiko ya kazi zao na kwamba Serikali kwa upande wake itaendelea kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.

Profesa Masannjila ameyasema hayo katika ufunguzi wa  maonesho ya sita ya Young Scientists Tanzania (YST) kwa  mwaka 2017 ambayo tangu kuanzishwa kwake  imeweza kuwashirikisha zaidi ya wanafunzi 1,410 kutoka shule mbalimbali hapa nchini.

Profesa Msanjila amesema nchi yetu inaongozwa na Dira ya Maendeleo ambayo inaelekeza kufikia uchumi wa kati inapofika mwaka 2025.

Ameongeza  kuwa mchakato unaofanyika hadi kufikia kipindi cha maonyesho  unajenga utamaduni wa kupenda Sayansi na kufanya Utafiti mashuleni.

Profesa Msanjila amesisitiza kuwa Wizara itaendelea kufanya kazi na Young Scientists Tanzania katika jitahada za kufikia malengo yake.

Amehimiza suala la kuwwpo kwa ushirikiano katika kujenga ndoto za wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi  ili wafikie malengo yao binafsi, na pia wafanikiwe kuchangia kutatua changamoto zinazoikabili jamii yetu.

Read 6566 times

Video News

Contact

  • Name:    Permanent Secretary
  • Address: 
  •               Mtaa wa Afya - Mtumba
  •               P.O.Box 10
  •               Dodoma
  • Tel:        +255 26 296 3533
  • Email:    Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.
  • Zonal SQA Offices Contacts
Top
We use cookies to improve our website. By continuing to use this website, you are giving consent to cookies being used. More details…